July 21, 2016

160719054611_rio_flag_russia_flag_624x351_afp



 

Wanariadha wa Urusi hawatashiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka huu huko Brazil.
Kauli hiyo imeafikiwa na mahakama ya juu ya michezo ambayo imefutilia mbali rufaa iliyowasilishwa na kamati ya olimpiki ya Urusi ROC ya kuitaka ibatilishe uamuzi wa shirikisho la riadha duniani IAAF wa kuwapiga marufuku wanariadha wake

wote wasishiriki michezo ya olimpiki itakayoandaliwa jijini Rio De Jenairo Brazil kuanzia mwezi ujao.
IAAF ilifikia uamuzi huo baada ya ufichuzi kuwa serikali ya Urusi ilikuwa na mpango wa chini kwa chini wa kuficha matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku miongoni mwa wanariadha wake.
Kamati ya olimpiki ya Urusi ilikuwa imekata rufaa kwa pamoja na takriban wanariadha 68 ambao hawajawahi kupatikana na hatia ya matumizi ya madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini.
Baada ya kusikiza pande zote mbili mahakama hiyo ya juu katika riadha CAS imeamua kufutilia mbali rufaa hiyo.
Kauli hiyo imewadia siku moja tu baada ya uchunguzi huru kubaini kuwa wizara ya michezo ya Urusi, na kamati ya kupambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu mwilini ya Urusi zilishiriki udanganyifu ikiwemo kubadilisha mikojo ya
wanariadha ilivipimo visipatikane na madawa hayo yaliyopigwa marufuku.
Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC imesema itatathmini kwanza hatua za kisheria, kabla ya kufanya uamuzi wowote kuhusu iwapo itaipiga marufuku Urusi kutoka kwenye mashindano ya Olimpiki huko Rio de Janeiro Brazil.
Hatua hii inafuatia ripoti huru kuhusu serikali kuhusika na kuwasaidia wanamichezo wake katika matumizi ya madawa ya kusisimua misuli.
IOC hata hivyo imewafungia maafisa wote wa Urusi kushiriki michuano ya Olimpiki ya Rio, na itawapima tena wanamichezo walioshiriki michuano ya Olimpiki ya majira ya baridi yaliyofanyika Sochi.
Tayari wanariadha wa Urusi wamepigwa marufuku na IAAF.
Shirikisho la riadha IAAF limefurahia kauli hiyo ya mahakama ya juu ya michezo ikisema kuwa imesawazisha uwanja wa riadha.
”Kwa hakika tumefurahi kuwa CAS imeunga mkono kauli yetu. Leo kwa hakika sio siku ya kufurahia kwani IAAF haikuja katika michezo kuwazuia wanariadha wasishiriki katika michezo ila nia yetu ni kusawazisha uwanja ili
wanariadha wote washindane kw mizani sawa” alisema rais wa shirikisho la riadha Lord Sebastian Coe.
”Baada ya rio tutaendelea kuisaidia kamati ya olimpiki ya urusi ilikuwaruhusu wanariadha wake kurejea katika mashindano ya kimataifa.” aliongezea Coe.
Licha ya uamuzi huo wa CAS,wanariadha wachache wa urusi ambao watakubali kushiriki chini ya bendera ya kamati ya olimpiki wataruhusiwa kushiriki ila lazima wapitie vipimo za ziada ilikuthibitisha kuwa ni wasafi.
Source: BBC

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE