July 01, 2016


Watu 11 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea leo na kuhusisha magari matatu eneo la Veta Dakawa mkoani Morogoro.
Watu 11 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali barabarani iliyotokea leo na kuhusisha magari matatu eneo la Veta Dakawa mkoani Morogoro.
Ajali hiyo imethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, ambaye amesema majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Morogoro kwa matibabu.
Ajali hiyo imehusisha basi la abiria mali ya kampuni ya Ota likitokea Bukoba kuelekea jijini Dar es Salaam, ambapo lori la mafuta lilikuwa linakwepa kontena lenye magunia ya mchele ndipo ikatokea ajali hiyo.
Hata hivyo Kamanda Matei amesema bado wanaendelea kufanya tathmini sahihi za idadi ya majeruhi na waliofariki katika ajali hiyo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE