Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) leo linaanza shamrashamra za
maandalizi kuelekea siku ya maadhimisho ya 52 ya majeshi inayotarajiwa
kufanyika Septemba Mosi mwaka huu kwa kufanya usafi na upandaji miti
katika kambi za jeshi na baadhi ya taasisi nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Msemaji wa
JWTZ Kanali Ngemela Lubinga aliwatoa hofu wananchi kuwa wasitishike
pindi watakapoona wanajeshi katika maeneo ya karibu na makazi yao.
“Kesho (leo) tuaanza kufanya usafi kuanzia maeneo ya Kawe hadi karibu na
kambi ya Lugalo, na kwamba niwatoe hofu wananchi pindi watakapoona
wanajeshi wengi mitaani kwa kuwa hatuna nia mbaya hivyo wasitufikilie
vibaya,” alisema.
Alisema jeshi hilo litafanya usafi pamoja na upandaji miti katika baadhi
ya maeneo nchini hadi siku ya kilele cha maadhimisho hayo. Pia
wanajeshi watajitolea damu salama katika hospitali za kambi za jeshi.
“Siku kuu ya majeshi itaadhimishwa pamoja na wanajeshi kujitolea damu
kwenye vituo maalumu vya kutolea damu salama mikoani, katika hospitali
zetu za kanda,” alisema na kuongeza.
“Sanjari na utoaji damu, madaktari wetu JWTZ watatoa huduma za tiba bure
kama upimaji wa virusi vya Ukimwi, kisukari, na upimaji wa shinikizo la
damu. “
“Kama ilivyo mila na desturi ya majeshi kufanya usafi na utunzaji wa
mazingira, kuelekea siku ya maadhimisho tutafanya usafi na kupanda miti
maeneo ya jirani na kambi na kwenye taasisi za kiraia kadri mahusiano
yatakavyofanyika na taasisi hizo, ” alisema.
Pia alisema siku hiyo ya maadhimisho itaadhimishwa kwa kuienzi michezo
na kudumisha urafiki baina ya JWTZ, wananchi, na Taasisi na kwamba
mashindano mbalimbali yatafanyika.
Tarehe hiyo hiyo ya Septemba 1 , Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA) kimetengaza kufanya maandamano na mikutano nchi nzima ili
kulaani kile wanachokiita udikteta unaofanywa na serikali ya awamu ya
tano.
Tayari tangazo hilo la Chadema limepingwa vikali na Rais John Magufuli,
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim, Mwigulu Nchemba, Waziri wa Mambo ya Ndani
na Nsato Marijani, Kamishina wa Jeshi la Polisi, Operesheni na Mafunzo
huku chama hicho kikiendelea kusisitiza azma yake.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment