Buchosa.
Mkazi wa Kijiji cha Kakobe, Kata
ya Kazunzu katika Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, Mkoa
Mwanza, Juma Abdallah (30) anadaiwa kuliwa na mamba na mabaki ya mwili
wake bado hayajapatikana.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kazunzu,
Thimothy Chuma alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Agosti 25
baada ya Abdallah akiwa na Hamisi Magayane wakivua samaki kandokando ya
Ziwa Victoria kurukiwa na mamba huyo na kutokomea naye.
Alisema baada ya kupata taarifa kutoka
Magayane (23), walipiga filimbi na wananchi kukusanyika kuanza kumsaka
mamba huyo, lakini hakupatikana.
Diwani wa Kata ya Kazunzu Boniphace
Msenyela aliwasihi wananchi kuendelea kumsaka mamba huyo, kwani
anapopata chakula hujificha katika miamba.
Msenyela alisema anaendelea kuwasiliana na maofisa wanyamapori ili kusaidia kumsaka mamba huyo.
Credit: Mwananchi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment