Amissi Tambwe akiinua mkono kushangilia baada ya kuifungia Yanga bao pekee leo

Kiungo wa Yanga, Thabani Kamusoko (kushoto) akimtoka beki wa MO Bejaia, Amar Banmelouka (kulia)

Winga wa Yanga, Obrey Chirwa (kushoto) akimtoka beki wa MO Bejaia, Amar Banmelouka (kulia)

Juma Abdul (kulia) akimtoka beki wa MO Bejaia, Zacharia Bencherifa

Simon Msuva akimtoka beki wa MO Bejaia, Zacharia Bencherifa
Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
YANGA SC imefufua matumaini ya kwenda Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kufuatia ushindi wa 1-0 jioni ya leo dhidi ya Mouloudia Olympique Bejaia ya Algeria katika mchezo wa marudiano Kundi A Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shukrani kwake, mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Josleyn Tambwe aliyefunga bao hilo pekee mapema tu kipindi cha kwanza.
Ushindi huo wa kwanza baada ya mechi tano, unaifanya Yanga ifikishe pointi nne baada ya awali kufungwa mechi tatu na kutoa sare moja ingawa inaendelea kushika mkia katika Kundi A.
Mazembe
inaongoza Kundi A kwa pointi zake 10 baada ya mechi nne, ikishinda tatu
na kutoa sare moja, ikifuatiwa na Bejaia na Medeama, ambazo kila moja
ina pointi tano za sare tatu na ushindi mmoja.
Tambwe
alifunga bao hilo dakika ya pili tu ya mchezo, akimalizia mpira
uliookolewa kufuatia Simon Msuva kuunganisha kwa kichwa krosi ya Juma
Abdul kutoka upande wa kulia.
Yanga sasa inaomba Medeama ya Ghana ifungwe na TP Mazembe kesho na baadaye ikatoea sare na MO Bejaia ili kwenda Nusu Fainali.
Yanga
ingeweza kuondoka na ushindi mnono leo, kama mshambuliaji wake, Obrey
Chirwa angekuwa makini na kutumia vizuri nafasi zaidi ya nne za wazi
alizotengenezewa.
Nafasi
iliyowasikitisha zaidi mashabiki wa Yanga ni ya kipindi cha pili,
Chirwa aliporuka kichwa cha mkizi baada ya krosi ya Simon Msuva kutoka
kushoto, lakini akapiga hewa akiwa amebaki na kipa, huku mpira ukienda
nje.
Kocha
Mholanzi, Hans van der Pluijm alilazimika kufanya mabadiliko ndani ya
robo ya kwanza ya mchezo, baada ya beki wake, Andrew Vincent ‘Dante’
kuumia na kumuingiza mkongwe, Kevin Yondan aliyemalizia vizuri mchezo.
Na
akalazimika pia kumpumzisha beki wake wa kulia, Juma Abdul baada ya
kipindi cha kwanza kufuatia kuumia nyama na kumuingiza kiungo Said Juma
‘Makapu’ aliyekwenda kucheza kama kiungo ea ulinzi, huku Mbuyu Twite
akihamia beki ya kulia.
Yanga
itahitimisha mechi zake za Kundi A Kombe la Shirikisho kwa kumenyana na
wenyeji TP Mazembe ya DRC mjini Lubumbashi Agosti 23, mwaka huu.
Kikosi
cha Yanga SC kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul/Said Juma
‘Makapu’ dk46, Mwinyi Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’/Kevin Yondan dk17,
Vincent Bossou, Mbuyu Twite, Simon Msuva, Thabani Kamusoko, Amissi
Tambwe, Obrey Chirwa na Deus Kaseke/Juma Mahadhi.
MO
Bejaia; Chamseddine Rahmani, Ismail Benettayeb, Faouzi Rahal, Sofiane
Khadir, Soumaila Sidibe, Zakaria Bencherifa, Mohamed Yacine Athmani,
Morgan Betorangal, Sofiane Baouali, Amar Benmelouka na Kamel Yesli
Kwa hisani ya binzubeiry
0 MAONI YAKO:
Post a Comment