August 24, 2016

Mwai Kibaki kufanyiwa upasuaji 

 Rais wa zamani wa Kenya Mwai Kibaki ambaye mapema wiki hii alisafirishwa Afrika Kusini katika hospitali ya  Netcare Sunninghill jijini Johannesburg atafanyiwa upasuaji mdogo .
Rais huyo wa zamani siku ya Jumapili alisafirishwa Afrika Kusini na madaktari wa AMREF baada ya kulazwa kwa muda mfupi katika hospitali ya Karen jijini Nairobi.
Ingawaje familia ya Kibaki hawakubainisha nini hasa kinamkumba rais huyo,madaktari wa Afrika Kusini wamesema kuwa anaendelea vizuri hadi kufikia sasa .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti la taifa la Daily Nation,Mwai atafanyiwa upasuaji wa shingo ambapo kipande cha damu iliyoganda katika mshipa wa damu kitaondolewa .
Aidha familia yake iliarifu kuwa Kibaki ataruhusiwa na madaktari kurudi nyumbani mwishoni na wiki hii na kuwaomba wakenya kuzidi kumuombea rais huyo mstaafu.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE