Licha
ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kutangaza kufanya
maandamano ya nchi nzima Septembe 1 2016, Jeshi la Polisi kanda maalum
Dar es salaam limemkamata mtu mmoja anayejulikana kwa
jina la Yoram Mbyellah kwa kupatikana na kuuza sare aina ya fulana zenye
maneno yanayodaiwa kuwa ni yakichochezi zikiwa na alama ya CHADEMA huku
nyingine zikiwa na maneno ‘UKUTA’
Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro amesema…>>>’August 20 2016 Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka
kwa raia wema kuwa maeneo ya Kinondoni kuna duka linauza flana zenye
maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA
UCHWARA’’ , ‘UKUTA’ ‘
‘Aidha
Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata
mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara na
mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake‘ –Kamanda Sirro
‘Ili
tuishi kwa amani ni lazima tutii sheria na kama hutaki kutii sheria
tutashughulika naye, Kama kuna mtu anataka kuvunja amani katika mkoa
wetu ajue kabisa hatoweza na niseme tu kwamba kama wanataka kujenga
ukuta wajenge ukuta mwingine maana huu umeshadondoka‘ –Kamanda Sirro
‘Na wapo watu wanasema
kwanini tunafanya mazoezi, nikwamba Jeshi la Polisi ni kawaida kufanya
hivyo na muhimu watu wajue hiyo September 1 hakutakuwa na maandamano ya
aina yoyote kwahiyo watu wasiwe na hofu bali wachape kazi‘ –Kamanda Sirro
0 MAONI YAKO:
Post a Comment