September 11, 2016

majeruhi

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi, amesema watu 13 wamefariki dunia na wengine  zaidi ya 200 wamejeruhiwa katika tukio hilo ambako lilizusha taharuki kwa wananchi wengi wa mikoa ya Kagera na Mwanza.
Kamanda Ollomi amesema mpaka sasa bado kikosi cha uokoaji cha zimamoto na chama cha msalaba mwekundu, wanaendelea na zoezi la kuwatafuta watu waliofunikwa na vifusi katika nyumba zilizoanguka kutokana na tetemeko hilo.

Hata hivyo, Kamanda Ollomi amesema ataendelea kutoa taarifa za tukio hilo pale atakapopata habari kutoka maeneo mengine yalikoathirika na tetemeko hilo mkoani humo.
Naye Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa tetemeko hilo mkoani mwanza, lakini hakuna madhara yoyote yaliyoripotiwa kutokana na janga hilo.
Nchi za jirani na Tanzania za Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya nazo pia zilikumbwa na kishindo cha tetemeko hilo lililotokea jana katika Ziwa Viktoria lililokuwa na ukubwa wa ritcher 5.7. – EATV

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE