September 11, 2016

magufuli-620x400
Rais wa Jahmuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesitisha safari yake ya kwenda nchini Zambia kutokana na maafa yaliyotokea mkoani Kagera.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 12 Septemba, 2016 alitarajiwa kuwasili Mjini Lusaka nchini Zambia kwa ziara ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine angehudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zitakazofanyika keshokutwa tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.

 Baada ya kuahirisha safari hiyo, Rais Magufuli atawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, 2016 limesababisha vifo vya watu 16 na kucha wengine 250 wakiwa majeruhi.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE