Picha za maji ya mto Daldykan ambayo yamebadilika rangi zimesambazwa sana katika vyombo vya habari Urusi.

Gazeti
la serikali la Rossiiskaya Gazeta linasema kuvuja kwa bomba la
kusafirisha taka za mchanganyiko wa shaba nyekundu na nikeli huenda
likawa kiini cha maji hayo kubadilika rangi.
Norilsk Nickel ndiyo mzalishaji mkubwa zaidi wa nikeli na palladium duniani.
Kampuni hiyo ina vinu na tanuri nyingi
rasi ya Taimyr eneo la Krasnoyarsk katika jimbo la Siberia. Ujenzi wa
vinu hivyo vikubwa ulifanyika enzi za muungano wa Usovieti.
Kampuni hiyo ina kiwanda kwa jina
Nadezhda karibu na mto Daldykan lakini maafisa wake wanasema hawajapata
dalili zozote za uchafuzi kutoka kwa kiwanda hicho.
Rais wa kampuni hiyo ni bilionea Vladimir Potanin.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment