Kikosi cha uokozi nchini Afrika Kusini,
kimeendelea na shughuli za kuwaokoa wachimba madini waliokwama katika
mgodi wa Langlaagte kwa siku kadhaa sasa.
Idara ya matukio yasiyotarajiwa nchini Afrika Kusini imesema
kuwa, wafanyakazi wake wa operesheni za uokozi wanaendelea na juhudi za
kuwatafuta wachimba madini haramu ambao tangu siku ya Jumatano iliyopita
wamekwama katika njia za chini ya ardhi katika mgodi uliofungwa
mjini Johannesburg.
Njia za chini ya ardhi katika mgodi wa madini
Idara hiyo imesema kuwa hadi sasa idadi ya wachimba migodi hao
waliokwama bado haijafahamika. Hii ni katika hali ambayo hadi sasa
waokoaji wamefanikiwa kuwaondoa watu wanne kutoka chini ya ardhi na
tayari kuna khofu kwamba wachimba mgodi waliosalia wamekwishafariki
dunia. Mgodi wa madini wa Langlaagte ni wa kwanza kugunduliwa mwaka 1886
mjini Johannesburg, hata hivyo imepita miaka kadhaa ukiwa umefungwa.
Mchimbaji wa dhahabu wakiwa chini ya miamba ya mawe
Maelfu ya wachimba migodi kinyume cha sheria wamekuwa wakipita njia
za chini ya ardhi na mashimo yaliyowahi kuchimbwa dhahabu kwa lengo la
kutafuta dhahabu kwenye mgodi huo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment