Mgogoro
unaoiandama CUF huenda ukailetea balaa zaidi, baada ya kuwapo kwa
taarifa kuwa huenda ikafutwa kama itazidi kukomalia msimamo ilionao wa
kutotaka ushauri.
Mgogoro
huo umekipasua chama hicho na kuwa makundi mawili, moja likiongozwa na
Profesa Ibrahim Lipumba na jingine likiwa chini ya Katibu Mkuu, Maalim
Seif Sharif Hamad.
Profesa
Lipumba aliyevuliwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi amejitwalia
ofisi kuu za chama hicho zilizopo Buguruni jijini Dar es Salaam, wakati
Maalim Seif na wanaomuunga mkono wako makao makuu ya chama hicho Vuga
visiwani Zanzibar.
Msajili
Msaidizi Sisty Nyahoza kupitia mahojiano yake na kituo cha Channel Ten,
ametumia nafasi hiyo kumtambua Profesa Lipumba kuwa bado ni mwenyekiti
halali wa CUF na kwamba ofisi hiyo inayo mamlaka ya kukifuta chama
chochote.
Alipoulizwa
kuwa migogoro hii inayoendelea haiwezi kusababisha chama kikafutwa,
Nyahoza amesema vipo vyama viwili vilivyowahi kufutwa usajili wake kwa
sababu ya migogoro ya uongozi na kuvitaja vyama hivyo kuwa ni chama cha
Pona kilichofutwa Mei 2001.
“Kilikuwa
na mgogoro wa uongozi, ambao ulifanya washindwe kufanya uchaguzi wa
viongozi wa kitaifa, kingine ni chama cha TPP, vilifutwa kwa hivyo
migogoro inaweza ikavunja chama na kikafutwa,” amesema.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment