October 07, 2016

makonda-26

Said Ally akiwa katika hali ya huzuni baada ya kuambiwa haotoona tena.



makonda-19 
…akifarijiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam, Paul Makonda.makonda-23 
…Akizungumza na Mhe. Makonda.
Mapema leo Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa majibu kuhusu na hatma ya kijana Said Ally aliyetobolewa macho na Scorpion maeneo ya Buguruni Sheli na kusema hatoweza kuona tena.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu huyo wa mkoa amesema:
“Majibu yametoka na Said ameturuhusu tuyaweke wazi majibu ni mabaya ila tumeyapokea itabidi tukubaliane na matokeo kwamba ndugu yetu hataweza kuona tena kwa maisha yake yote.
“Serikali ya mkoa imejitolea kumpatia matibabu ya macho ya bandia kwa ajili ya kutengeneza shape ya uso wake tena, kumpatia elimu ya kusoma tena kujifunza kwa alama ili aweze kuendana na mazingira. Serikali ya mkoa imetoa gari kwa ajili ya kumsaidia kipindi chote atakachokuwa kwenye matibabu yake.
“Kabla ya kupatwa na ulemavu huo, Said alikuwa kinyozi hivyo kuna mdogo wake yupo atamsaidia kwakuwa mwanzoni walikuwa wakifanya kazi pamoja.”
Na Hilaly Daud/ GPL.

                     

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE