Wanasayansi wameonya kuwa wale ambao hupenda kujipiga selfie mara kwa mara, wana hatari ya kuwa wapweke.Wanadai inaweza kuwa ni ishara ya kuwa na matatizo kwenye mahusiano yao au tatizo la afya ya akili.
Wanaojipiga sana selfie wanaweza kuwa watu wenye kasoro au wanaotafuta kuangaliwa, utafiti umesema. Watafiti nchini Thailand, walifanyia tathmini wanafunzi 300 na kuangalia mara ngapi huangalia picha walizojipiga wenyewe.
Washiriki hao ambao wengi walikuwa wanawake, walikuwa na umri kuanzia miaka 21 hadi 24, walihojiwa kuangaliwa kama walikuwa ni watu wa kujiamini, kutaka kuonekana, tabia ya kuwa wenyewe au upweke.
Wengi wao walionekana kutumia asimia 50 ya muda wao wa ziada katika simu zao au kwenye internet.
Wataalam wanaamini kuwa wanaume na wanawake wenye upweke hupenda kuchukua zaidi selfie kutafuta kukubalika na watu wengine.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment