October 10, 2016

Na Julius S. Mtatiro
 
Mahakama kuu Ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Leo tarehe 10/10/2016 imetoa ushindi kwa Chama cha Wananchi (CUF) kwa kutoa kibali cha kisheria kwa chama kuwasilisha ndani ya siku 14, kesi ya kuiomba mahakama kutengua maamuzi batili ya Msajili wa vyama vya Siasa nchini, kwani maamuzi hayo batili yametengua maamuzi halali ya vikao halali vya chama. Mawakili wa CUF wakiongozwa na Mhe. Juma Nassor, Mhe. Daimu na Mhe. Hashim Mziray wamewaahidi wanachama wa CUF nchi nzima kwamba wataifungua kesi husika ndani ya wiki hii. Kwa kawaida, uamuzi wa leo wa Jaji Munisi huweza kufanywa upande mmoja (EXPARTE) kama ilivyofanyika.
#MyTake:
Hili ni pigo la kwanza kwa Lipumba na kibaraka wake Mtungi. Kitendo cha Mahakama kuruhusu suala hili kujadiliwa mahakamani ni dalili za haki kutendeka. Baada ya CUF kuwasilisha ushahidi wake ndani yasiku 14 kama ilivyoelezwa, na ikiwa Mahakama itakubaliana na hoja za CUF kuwa Lipumba si Mwenyekiti wa Chama hicho, sijui Mtungi ataficha wapi sura yake. #Shame.!

Wakati huohuo:
PROF Lipumba Agonga Mwamba..Sakata la Kufungua Account Mpya ya Bank

PROFESA Ibrahim Lipumba amegxonga mwamba. Juhudi zake za kufungua akaunti ya benki, tofauti na iliyo halali na inayotumika, zimekwama, anaandika Shabani Matutu.
Prof. Lipumba anadaiwa kutaka kufungua akaunti yake katika Tawi la Ilala la National Microfinance Bank (NMB) jijini Dar es Salaam.
Prof. Lipumba ambaye kwa miezi miwili sasa amekuwa akinyukana na uongozi halali wa Chama cha Wananchi (CUF).

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE