Baadhi ya wafanyakazi wa NMB
waliofika kwenye maonyesho hayo wakitoa ufafanuzi wa jambo kwa Waziri
Mwinjage (kushoto) na Waziri Dk.Mpango.
..Dk.Mpango akisoma hotuba yake katika hafla hiyo.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa NMB, James Metairon naye akizungumza jambo.
Ofisa wa Kitengo cha Uongozaji wa Imori International, Matrina Ambrozy akieleza jambo katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Imori International,
Leo Mukirya (kushoto) akimtembeza Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha
Uwekezaji Tanzania, Patrick Nkandi (kulia).
Baadhi ya bidhaa iliyopo kwenye maonyesho hayo.
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk.Philip Mpango, leo ameipongeza benki
ya NMB kwa juhudi zake inazozionesha katika utoaji wa mikopo na riba
nafuu kwa wajasiliamali wadogo.
Hayo ameyasema leo katika ufunguzi wa maonyesho ya sekta ya kibenki na fedha yaliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Hayo ameyasema leo katika ufunguzi wa maonyesho ya sekta ya kibenki na fedha yaliyofanyika katika viwanja vya Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika hafla hiyo Dk. Mpango amewapongeza waandaaji wa
maonyesho hayo ambao ni Imori International kwa kuona umuhimu wa
kuanzisha utaratibu wa maonyesha katika sekta ya fedha katika maendeleo
ya viwanda na uchumi kwa taifa ambapo ndio yameanza kwa mwaka huu.
Amesema, serikali kwa kupitia wizara ya fedha na mipango, wizara ya viwanda na biashara inawahakikishia kuwapa ushirikiano katika kuendeleza utaratibu mzuri.
Amesema, serikali kwa kupitia wizara ya fedha na mipango, wizara ya viwanda na biashara inawahakikishia kuwapa ushirikiano katika kuendeleza utaratibu mzuri.
“Kwanza napenda nitoe pongezi kwa benki ya NMB PLC (National
Microfinance Bank Plc) kwa kuona umuhimu wa kudhamini maonyesho haya
kwani udhamini huu umetupatia wote fursa ya kukutana na kuonyesha jamii
huduma zinazotolewa na sekta ya fedha na shughuli za wajasiliamali ambao
wana kiu kubwa ya mitaji ili kwa pamoja tushirikiane kujenga Tanzania
ya viwanda,” alisema.
Akaongeza: “Serikali inatambua mahitaji makubwa ya kufanya maboresho
na kuwezesha mabenki na taasisi nyingine za kifedha kuweza kufikia watu
wengi kwa maana ya mitaji ya kutosha ya kuongeza uwekezaji wa ndani.
“Serikali imedhamiria kuweka msukumo zaidi kujenga mazingira rafiki kwa wadau wa sekta hi ili iweze kupanua huduma zake hapa nchini na hivyo kuchochea uzalishaji na upatikanaji wa huduma bora za jamii,” Aidha amewataka waandaaji kufanya maonyesho hayo katika mikoa mingine ili hata kule ambapo taasisi hizi za kifedha na benki ni chache, basi zipate hamasa kuwekeza huko kama chachu ya maendeleo ya taifa.

Alitoa msisitizo kuwa mbali na mabenki hayo kufanya biashara, hivyo
ni wajibu kwa wajasiliamali nao kwenda wakiwa na miradi mizuri
inayokopesheka na wakipata mitaji basi waitumie ilivyokusudiwa na waweze
kurudisha kwa wakati muafaka.
Kauli mbiu ya maonyesho hayo ilikuwa ni “Fursa Katika Dunia ya Kifedha”
Kauli mbiu ya maonyesho hayo ilikuwa ni “Fursa Katika Dunia ya Kifedha”
0 MAONI YAKO:
Post a Comment