Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Fc, Yusuph Manji leo amefunguka kuhusu taarifa za uwepo wa mgogoro wa eneo alilolitoa kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo lililopo Gezaulole na kusema kuwa eneo hilo halina mgogoro na kwamba wakati wowote wanachama wa klabu hiyo wakimpa ridhaa, ujenzi wa uwanja huo utaanza baada ya siku tisini.
Manji ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandilizi ya mkutano mkuu wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika Oktoba 23, 2016.
Amesema kuwa, hati ya eneo hilo imeandikwa jina la Kampuni yaani Yanga Yetu, pia amefafanua kuwa eneo litakalotumika kwa ajili ya ujenzi wa uwanja huo haliko katika mgogoro wowote.
“Uwanja wa mazoezi utaanza kujengwa ndani ya siku tisini pindi wanachama wakituruhusu, na ujenzi wake hautachukua zaidi ya miezi nane,” amesema Manji.
Amesema kuwa “Nataka uwanja wa mpira na mazoezi ujengwe tofauti, natumaini wanachama wa Yanga watanikubalia ombi langu ili nianze ujenzi mapema.