October 22, 2016

yusuph-manji

MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji ameahirisha mkutano wake na wanachama wa klabu hiyo uliotarajiwa kufanyika kesho Jumapili kufuatia kupokea barua ya zuio la mkutano huo kutoka kwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wanachama wawili wa klabu hiyo Juma Magoma na aliyewahi kuwa mwansheria wa klabu hiyo, Frank Chacha ndiyo walioiomba mahakama hiyo izuie mkutano huo uliopangwa kufanyika kwenye Makao Makuu ya klabu hiyo yaliyopo Jangwani jijini Dar.

Manji ametoa tamko hilo la kuahirisha kwa mkutano huo limetolewa leo kwenye makao makuu ya klabu hiyo na kudai kuwa hawezi kuingilia uhuru wa mahakama kwani anaamini suala hilo litaisha na atatangaza tarehe nyingine ya kufanyika kwa kwa mkutano huo mara baada ya taratibu zote za kimahakama kukamilika.

Aidha Manji amewataka wanachama wa klabu hiyo kuwa wavumilivu huku akiwaomba wanachama waliokuwa watokee mikoani kuacha kuja jijini Dar es Salaam hadi hapo atakapotangaza upya.


                     

Related Posts:

  • LIVE: Barcelona VS Juventus   Muda huu kuna mpambano unaoendelea kati ya Barcelona na Juventus. Tumekuwekea hapa waweza kufwatilia mpaka mwisho ili uweze kujua nini kinajiri katika mpambano huu        &nbs… Read More
  • Kuhusu Point 3 za Kagera, Simba yaivaa TFF   Klabu ya Simba leo imeibuka na kupinga utaratibu unaotumiwa na TFF katika kushughulikia suala la pointi 3 ilizopewa kutoka klabu ya Kagera Sugar kwa kosa la kumchezesha mchezaji aliyekuwa na kadi 3, huku… Read More
  • Point za mezani na Mitazamo ya Rage Ismail Aden Rage-Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba SC Mwenyekiti wa zamani wa Simba Alhaj Aden Rage ameungana na wadau wengine kupinga matokeo ya mezani kwakua kuna njia nyingi za kuweza kuepuka timu kupewa au kupokw… Read More
  • Tweet ya Prof. J kuhusu Millard Ayo hii hapa   Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya CHADEMA Joseph Haule Prof, J, amempongeza mtangazaji wa Clouds Media Millard Ayo kwa kutoa habari zake na kupaza sauti za wanyonge.  Prof J ametweet leo hii  Joseph L.… Read More
  • Mwizi wa simu anaswa kwa kutumia App   Mshukiwa wa wizi ambaye inaaminika alikuwa ameiba zaidi ya simu 100 aina ya iPhones amekamatwa nchini Marekani. Mwizi huyo alikamatwa baada ya watu waliokuwa wameibiwa simu zao kutumia programu tumishi ya Find My … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE