
Chama
Cha Walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Singida, kimeiomba serikali ya Rais
Magufuli kwamba baada ya kumaliza uhaba wa madawati, nguvu zake
izielekeze katika kumaliza kulipa madeni ya walimu yakiwemo ya mishahara
na yale yasiyokuwa ya mishahara.
Ombi
hilo limetolewa jana na mwenyekiti wa CWT mkoa wa Singida, Allani
Jumbe, wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili ya
kuwajengea uwezo waweka hazina wa ngazi ya vitengo walimu wanawake,
kutoka mikoa ya Singida, Dodoma, Manyara, Pwani na Dar es Salaam.Mafunzo
hayo yanafanyikia ukumbi wa mikutano wa ofisi CWT mkoa wa Singida.
Alisema serikali chini ya
uongozi wa rais Dk.Magufuli, imefanya kazi nzuri ya kumaliza uhaba wa
madawati katika shule za msingi na sekondari kwa kiwango kikubwa.
“Sasa wanafunzi wetu
wamejengewa mazingira mazuri ya kujifunzia ili taaluma iweze kupanda kwa
kiwango stahik, ni muda sasa serikali kuelekeza nguvu zake katika
kumaliza kulipa madeni ya walimu,” alifafanua Jumbe.
Aidha, alisema tatizo la walimu
kupandishwa madaraja na kurekebishiwa mishahara yao kulingana na ngazi
zao nalo litafutiwe ufumbuzi wa kudumu.
“Hivi karibuni kumetokea kituko
cha aina yake, baadhi ya walimu walipandishwa madaraja, wengine
mishahara yao ikarekebishwa na wengine mishahara yao haikurekebishwa
kabisa. Baada ya muda mfupi wale ambao mishahara yao ilirekebishwa,
marekebisho hayo yakafutwa na kunyang’anywa fedha walizokuwa
wamelipwa”,alisema.
Na Nathaniel Limu, Singida
0 MAONI YAKO:
Post a Comment