
Donald Trump hayupo tayari kuyakubali matokeo ya urais wa Marekani – iwapo akishindwa of course.
Mgombea wa Urais wa Marekani wa chama cha Republican, Donald Trump akizungumza kwenye mdahalo wa tatu uliofanyika Jumatano
Katika mdahalo wa tatu na wa mwisho uliofanyika Jumatano hii, mgombea
huyo kupitia chama cha Republican, amesema ana wasiwasi kura zitaibiwa.
Amedai kuwa mpinzani wake, Hillary Clinton wa chama cha Democratic,
hakutakiwa hata kuwania nafasi hiyo.
Mgombea wa Urais wa Marekani wa chama cha Democratic, Hillary Clinton akizungumza kwenye mdahalo huo
Alikuwa akielezea kuhusu kashfa ya barua pepe iliyomgubika Clinton, ambayo amekuwa akiitumia kila wakutanapo. Kwa kauli yake, Trump ameonesha dhahiri kuwa hatokubaliana na matokeo ya uchaguzi huo utakaofanyika Nov. 8.

Kaka yake Barack Obama, Malik alikuwepo kwenye mdahalo huo kwa mwaliko wa Trump, mgombea anayemuunga mkono
“Every time Donald thinks things are not going in his direction, he claims whatever it is, it is rigged against him,” alisema Clinton. “The FBI conducted a yearlong investigation into my emails that concluded there was no case. There was even a time when he didn’t get an Emmy for his TV program three years in a row, and he started tweeting that the Emmys were rigged,” aliongeza Clinton.

Trump akiongozana na mkewe Melania kuingia kwenye mdahalo huo
Mwisho wa mdahalo huo, Clinton alisusa kumpa mkono mpinzani wake.
Kwa mujibu wa kura za maoni za CNN za watu waliotazama mdahalo huo, Clinton ameshinda kwa mara ya tatu kwa kupata 52% na Trump kupata 39%.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment