November 09, 2016

4k0a2514

Jukwaa kubwa la mitindo Afrika Mashariki na Kati, Swahili Fashion Week 2016 limepangwa kufanyika December 2016 huku likitarajia kuwakutanisha zaidi ya wabunifu 40 kutoka Afrika Mashariki na kati.
Maonyesho hayo ambayo yatafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Posta jiji Dar es salaam kuanzia December 2 na 3, yatakuwa ya aina yake kutokana na wabunifu hao kutaka kuonyesha mapinduzi makubwa ya mitindo nchini.
Akiongea na waandishi wa habari Jumatano hii, Mkurugenzi wa Swahili Fashion Week, Mustafa Hassanali, amesema mwaka huu wameyafanya maonyesha hao kuwa yenye hadhi ya kimataifa.
“Si kwamba tu tuionyeshe dunia kuwa Tanzania kuna vipaji vya ubunifu lakini nafasi hii itatusaidia kuiweka Tanzania katika ramani ya ubunifu kutoka na kuwepo kwa vyombo vikubwa vya habari vya kimataifa,” alisema Mustafa.Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA), Godfrey Mngereza ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo, alisema serikali inaunga mkono juhudi za maonyesho hayo kwa kuwa yanaitanga nchi.
“Suala la ubunifu linakuza utamaduni, hata ukiangalia nembo ya mwaka huu ambayo imepambwa rangi za Tausi hiyo moja kwa moja imekuza utamaduni wa Tanzania. Lakini pia imekuza rasilimali za nchini ya Tanzania ambazo tunazo, kwahiyo mbunifu huyu ametupeleka Tanzania katika kiwango cha kimataifa ili waweze kuona utamaduni tulionao,” alisema Ngereza.


                          

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE