May 28, 2017

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa anaongea na Mzee Ngosha
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli leo 28 Mei 2017 amefanya ziara katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwatembelea na kuwajulia hali wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo. Akiambatana na mkewe Mama Janeth Magufuli, Rais Magufuli aliwajulia hali wagonjwa mbalimbali wakiwemo Mzee Francis Maige Kanyasu (Ngosha) anayesemekana kwamba ndiye aliyechora Nembo ya Taifa  pamoja na mtoto Shukuru aliyekuwa 
akiishi kwa kunywa mafuta na sukari.
  
Rais Magufuli na Mkewewakimjulia hali Mtoto Shukuru aliyekuwa akiishi kwa kunywa mafuta na sukari

“Jamani, Madaktari tunawashukuru sana, mnafanya kazi nzuri, Madaktari wote nchini pokeeni pongezi zangu, sisi serikali tutaendelea kuzikabili changamoto hizo na siku moja zitakwisha. Kikubwa ni kumtanguliza Mungu mnapofanya kazi ya kuokoa maisha ya watu kwa juhudi kubwa, mnafanya kazi ya Mungu” alisema Rais Magufuli.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru ameweza kumshukuru Rais Mgufuli kwa kuwatembelea huku akisisitiza kuwa tayari madaktari wamegundua magonjwa yanayomkabili Ngosha pamoja na Mtoto Shukuru.
Aidha, Prof. Museru amesema hospitali hiyo imepiga hatua kubwa ya kujenga uwezo wa kutibu magonjwa ambayo wagonjwa walilazimika kwenda kutibiwa nje ya nchi na hivyo kuokoa fedha nyingi za serikali.
 
“Mhe. Rais hospitali yetu sasa imeanza kufanya upasuaji na kutoa tiba ya magonjwa ambayo yalilazimu wagonjwa kwenda kutibiwa nje ya nchi, mfano hivi sasa tunatoa huduma ya kusafisha figo kwa wagonjwa takribani 250, na kuanzia mwezi Julai mwaka huu tutaanza kupandikiza figo.Huduma hii hugharimu kati ya Shilingi Milioni 60 na Shilingi Milioni 70 kwa mgonjwa mmoja anayekwenda kutibiwa nje ya nchi, lakini hapa nchini gharama zinashuka hadi Shilingi Milioni 21” alisema Prof. Museru.
 

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE