May 29, 2017

media 

Korea Kaksazini imefanya tena jaribio la kombora la masafa mafupi kuelekea Japan. Kombora hili ni la tatu kurushwa na Korea Kaskazini katika kipindi cha wiki tatu.
Korea Kaskazini imeendelea kukiuka azimio la Umoja wa Mataifa linaloizuia kufanya majaribio yoyote ya makombora au silaha za nyuklia, na imeongeza kasi na idadi ya majaribio hayo katika miezi ya karibuni.
Kombora hili aina ya Scud lilipaa umbali wa kilomita 450 kabla ya kuanguka katika maeneo ya bahari ya Japan.
Kikosi cha Jeshi la Marekani Bahari ya Pasifiki kimesema kombora hilo lilirushwa kutoka Wonsan, Korea Kaskazini na lilipaa kwa karibu dakika sita kabla ya kuanguka.
Jariibo hilo la kombora limetekelezwa siku moja baada ya vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini kusema nchi hiyo lilifanyia majaribio mfumo mpya wa kudungua ndege za kivita, na kutoa picha za kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un alishuhudia majaribio hayo.
Itakumbukwa kwamba majaribio mawili ya ya hivi karibuni yaliyofanywa na Korea Kaskazini, ambayo ilisema yote yalifanikiwa, yalikuwa ya makombora ya masafa ya wastani na masafa marefu.
Korea Kaskazini ilisema jaribio la kwanza lilikuwa la kombora jipya lenye uwezo wa kubeba kichwa cha bomu la nyuklia.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE