Taifa Stars ambayo itakuwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kesho saa 7. 45 mchana inakwenda Misri kufanya kambi ya siku nane kujindaa na mchezo dhidi ya Lesotho utakaofanyika Juni 10, 2017 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji hao 21 kutoka hapa Tanzania wataungana na na wengine wawili, Nahodha Mbwana Samatta na Faridi Mussa wanaocheza ughaibuni katika kikosi hicho na kufanya jumla ya wachezaji kuwa 23 watakaokuwa nchini Misri. Tayari Thomas Ulimwengu wa AFC Eskilstuna – Sweden.
Nahodha Msaidizi,
Jonas Mkude hatakuwako kwenye msafara huo kutokana na ushauri wa
madaktari walioelekeza kwamba nyota huyo wa Simba apate mapumziko ya
angalau siku nne.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga ameridhia na kusema kuwa Mkude ataungana na wenzake Juni 8, mwaka huu timu itakaporejea kutoka Misri.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga ameridhia na kusema kuwa Mkude ataungana na wenzake Juni 8, mwaka huu timu itakaporejea kutoka Misri.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment