May 02, 2017

Image may contain: 9 people, people standing 

Image may contain: 4 people, people sitting

Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF-Maalim Seif Sharif Hamad Leo ameendelea na ziara yake kwa siku ya pili katika wilaya ya Kinondoni na Ubungo-Dar es Salaam kwa kuwatembelea Wazee wa CUF, kuwafariji Wagonjwa na wafiwa mbalimbali. Ziara hiyo ilianza majira ya saa 5:30 asubuhi katika Kata ya Mzimuni na Magomeni kwa kuwatembelea Mzee Lipaki, Bi. Mariam John, Mzee Shaaban Nassor na Bi Rihama. Akiambatana na madiwani wa UKAWA (CUF na CHADEMA) katika wilaya hizo akiwa wilaya ya Ubungo aliwatembelea Hassan Abdi (Makoka), Jasmini Mgonja (Mbezi Makabe), Mrs Levi kapinga (Stop-Over). Kata ya Msasani alikwenda kuhani msiba wa Mwanachama wa CUF muasisi Marehemu Fatma Ngonyani, na kumfariji Mzee Ally. Akiwa kata ya Kimara –Stopover alikaribishwa katika ofisi ya Serikali ya Mtaa ambapo alisalimiana na wajumbe wa Mtaa huo na viongozi mbalimbali na kusaini kitabu cha wageni, Mwenyekiti wa Mtaa huo Bi. Magreth Kyai Mugyabuso amemueleza Katibu Mkuu kuwa mtaa huo unaongozwa kwa mashirikiano ya vyama –UKAWA na kwamba anashirikiana vyema na wajumbe wake wa mtaa kuwahudumia wananchi.
Akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ambavyo vilijitokeza kufuatilia ziara hiyo Katibu Mkuu, Maalim Seif amesema kuwa “CUF haina mgogoro wowote kilichokuwepo ni upandikizi wa sintofahamu iliyoingizwa ndani ya CUF na Msajili wa Vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi, CUF na viongozi wake wote wapo makini na imara na wataendeleza mapambano ya kudai haki sawa kwa watanzania wote na kwamba haina muda wa kuzungumza na wasaliti na vibaraka kwa kuwa si wanachama wa CUF. Amewahakikishia wanachama na wananchi waliojitokeza kumpokea katika maeneo mbalimbali aliyoyatembelea kuwa muda si mrefu utulivu utapatikana na CUF itarejea katika hali yake ya kawaida.” Ameeleza kuwa Chama kitaandaa ziara rasmi ya ukaguzi wa shughuli na uhai wa Chama kwa Mkoa wa Dar es salaam na Tanzania Bara kwa ujumla.
Katika ziara yake hiyo msafara huo Katibu Mkuu aliambatana Mhe. Abdallah Mtolea (MB-Temeke, na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa), Mhe, Shaweji Mketo(Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi), Mhe. Mbarala Maharagande (Naibu Mkurugenzi wa Habari), Mhe. Juma Mkumbi (Mwenyekiti wa Wilaya ya Kinondoni na Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa), Mhe. Salma Mwassa (MB-V/Maalum), pamoja na Viongozi wengine. Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Ubungo Mhe. Said Kubenea ametuma Salamu za kumpongeza Katibu Mkuu, Maalim Seif kufanya ziara hiyo na kuwajulia hali wapiga kura wake, amesema kuwa alitamani sana kuwepo pamoja nae lakini amedharurika na shughuli za bunge zinazoendelea Mjini Dodoma. Katika kumuhakikishia usalama wake Katibu Mkuu akiwa Jimboni kwake Ubungo, Mhe. Kubenea ametoa vijana wake wa Ulinzi 26 walioungana na walinzi makini wa CUF (Blue Guards) kufanikisha ziara hiyo ambayo ilifanyika kwa utulivu, usalama na mafanikio makubwa.

Kesho Tarehe 3/5/2017 Mheshimiwa, Katibu Mkuu, Maalim Seif ataanza ziara yake kwa kutembelea Kituo Cha Habari- Clouds Media saa 1:30 asubuhi na kufanya mahojiano katika kipindi cha @360 na baadae kuzungumza na Menejimenti ya kituo hicho. Baada ya hapo ataendelea na ziara yake kwa siku ya tatu wilaya ya Temeke kuanzia saa 5 kamili asubuhi.

Haki Sawa Kwa Wote
Maharagande,
NMHUMU
2/5/2017

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE