Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad Leo ameanza Ziara Rasmi ya
siku tatu katika wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwatembelea Wazee
wa CUF, kuwafariji Wagonjwa na wafiwa mbalimbali. Ziara hiyo iliyoanza
majira ya saa 5 kamili asubuhi katika Kata ya Upanga ambapo alikwenda
kumjulia hali mjane wa Marehemu Imamu Mohamed Ali Abeid, baadae
alikwenda kumjulia hali Mzee Mawanja(Vingunguti), Mzee
Hussein Kutopa –Mratibu CUF (kata ya Vingunguti) , Sheikh Juma, Bibi
Hidaya, Hamad Tafiko, Mzee Mfaume (kata ya Gongolamboto), wengine
waliotembelewa na Katibu Mkuu ni pamoja na Mzee Kombo Faki, Yusuf Musa,
Mzee Hamisi (kata ya Majohe).
Akiwasalimu wananchi wengi waliojitokeza kwa furaha kubwa kumuona
Kiongozi wao katika maeneo mbalimbali aliyofika, Maalim Seif
amewahakikishia kuwa CUF ni Taasisi Imara na kamwe haiwezi kuyumbishwa
na mtu yeyote yule, na kwamba itazishinda changamoto zote zilizojitokeza
muda si mrefu. Amewataka vijana kujiandaa kwenda kuchukua ofisi yao ya
Buguruni wakati wowote kuanzia sasa.
Katika msafara huo Katibu Mkuu aliambatana na Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe Musa Kafana, Naibu Meya wa Ilala Mhe. Omari Kumbilamoto, Mhe. Abdallah Mtolea (MB-Temeke, na Naibu Mkurugenzi wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa), Mhe, Shaweji Mketo(Naibu Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi), Mhe. Mbarala Maharagande (Naibu Mkurugenzi wa Habari), Mhe. Bakari Shingo ( Mwenyekiti wa Wilaya ya Ilala), Mhe. Salma Mwassa(MB-V/Maalum), pamoja na Viongozi wengine mbalimbali wa Jumuiya za Chama na Walinzi (Blue Guards).
Mheshimiwa, Maalim Seif ataanza ziara rasmi ya ukaguzi wa uhai na shughuli za Chama katika Mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara kwa ratiba itakayotolewa hivi karibuni.
Haki Sawa Kwa Wote
Maharagande,
NMHUMU
1/5/2017

0 MAONI YAKO:
Post a Comment