May 01, 2017

Image result for jacob zuma 
 
Rais wa Afrika Kusini anayekumbwa na kashfa Jacob Zuma, ameondoka kwenye mkutano wa siku ya kimataifa ya wafanyazi baada ya kukemewa na wafanyakazi wanaomtaka ajiuzulu.
Fujo zilizuka kati ya wafuasi wa Bwana Zuma na wapinzani na kusabababisha hotuba yake kufutwa.
Chama kikuu cha wafanya kazi Cosatu, kilimtaka Bwana Zuma ajiuzulu mwezi uliopita baada ya kumfuta kazi waziri wa fedha alijekuwa akiheshimiwa sana.Bwana Zuma ameapa kusalia ofisini hadi muhula wake ukamilike mwaka 2019

 Maandamano yamekuwa yakifanyika kumtaka Zuma ajiuzulu 
Maandamano yamekuwa yakifanyika kumtaka Zuma ajiuzulu
 
Alionyeshwa na runinga akiondoka jukwaani kwa hasira na kuondolewa na magari kutoka kwa mkutano ulioandaliwa mjini Bloemfontein
Maafisa wa vyeo vya juu wa ANC nao walikemewa kwenye mkutano uliofanyika mjini Durban.Shinikizo za kumtaka Zuma ajiuzulu zimekuwa zikoongezeka tangu amfute kazi waziri wa fedha Pravin Gordan mwezi Machi.
 

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE