
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili mjini Arusha ambapo
leo ataongoza wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani katika
kuaga miili ya wanafunzi 32,walimu Wawili pamoja na dereva Mmoja wa
shule ya Lucky Visent iliyopo Jijini Arusha waliopata ajali tarehe
06-May-2017 katika eneo la Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha.
Ibada na dua za kuaga miili ya marehemu hao itafanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha kuanzia Saa Mbili asubuhi hii leo.
Katika uwanja wa ndege wa Arusha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na ujumbe wake wamepokelewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo pamoja na Viongozi wa wengine wa mkoa huo.
Mungu azipumzishe roho zao Mahala pema peponi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment