Matokeo ya awali yameanza kutangazwa nchini
Ufaransa ambapo kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa na wizara ya mambo ya
ndani ya Ufaransa yanaonesha mgombea Emmanuel Macron anaongoza kwa
asilimia 65.1 dhidi ya asilimia 34.9 aliyopata Marine Le Pen.
Muda mfupi uliopita Marine Le Pen
amewahutubia wafuasi wake na kutangaza kumpongeza Macron kwa ushindi
alioupata huku akisema uchaguzi huu umekuwa ni wa kihistoria.
Le Pen amesema matokeo haya yametoa taswira mpya kwa siasa za Ufaransa ambapo amewashukuru wapiga kura wake kwa kumuunga mkono toka kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi.
Kiongozi huyo ameongeza kuwa yeye ataongoza upinzani bungeni ili katika kuhakikisha nchi yao inarejea kwenye ramani ya dunia.
Taarifa za ndani zinasema kuwa Macron pia alimpigia Marine Le Pen na kumpongeza kwa upinzani aliouonesha wakati wa kipindi chote cha kampeni.
Ushindi wake unamaliza miezi kadhaa ya hofu waliyokuwa nayo viongozi wa jumuiya ya Ulaya ikiwa mgombea Marine Le Pen angeshinda kwenye kinyang’anyiro cha mwaka huu.
Viongozi mbalimbali wa dunia wameendelea kutuma salamu za pongeza kwa raia wa Ufaransa na Emmanuel Macron wakimpongeza kwa ushindi wake waliosema ni wa kishindo.
Rais wa Ufaransa anayemaliza muda wake Francois Hollande amempongeza Macron kwa ushindi wake na kumtakia kheri.
Kansela wa Ujerumani na rais wa tume ya umoja wa Ulaya Jean Claude Junker nao wametuma salamu za pongezi kwa Macron wakiwashukuru wananchi wa Ufaransa kwa kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua mpenda mabadiliko na kiongozi anayeona Ulaya mpya.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment