DCP Ahmed Msangi
Mwanamume mmoja mkazi wa Mahina wilayani Nyamagana mkoani Mwanza amemuua
mkewe kwa kumpiga risasi na yeye mwenyewe kujiua baada ya kutokea
ugomvi baina yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP
Ahmed Msangi amewataja watu hao kuwa ni Maximilian Ngedere (40) na Tedy
Patrick (38) ambapo ugomvi baina yao ulianza baada ya wawili hao kurudi
kutoka katika biashara zao, majira ya saa 4:15 usiku wa tarehe 25 Mei,
2017.
Inadaiwa kuwa wawili hao ambao ni
wafanyabiashara ya samaki walipofika nyumbani ulitokea ugomvi na pindi
ugomvi huo ukiendelea kulisikika milio ya risasi kutoka chumbani.
Kamanda Msangi amesema Max alimjeruhi
mkewe kwa kumpiga risasi sehemu ya mgongoni, kisha kujipiga na yeye
mwenyewe risasi ya kifuani, hali iliyopelekea yeye mwenyewe kufariki
dunia papo hapo huku mkewe akijeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya rufaa
ya Bugando akiwa na hali mbaya na ilipofika leo majira ya saa 3 asubuhi,
akafariki dunia.
Amesema chanzo cha mauaji hayo bado
kinachunguzwa na kwamba polisi wapo katika upelelezi kuhusiana na mauaji
hayo wakati miiliyao ikiwa imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya
Bungando kwa uchunguzi zaidi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment