John Bocco
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na Azam FC ya Tanzania John Bocco
ameachana rasmi na klabu yake hiyo aliyoitumikia kwa muda mrefu kwa
mafanikio makubwa.
Nahodha
huyo wa zamani wa Azam FC na taifa Stars ameondoka Azam FC akiwa kama
mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na matajili hao wa jiji la
Dar es Salaam wakitumia dimba la Azam Complex.
Kwa mujibu wa uongozi wa Azam FC kupitia
kwa afisa habari wa timu hiyo Jafar Idd Maganga wamethibitisha kuondoka
kwa mchezaji huyo kwani hawakuwa na mkataba naye tena.
Amesema "Kimsingi Azam FC inatangaza
rasmi kuwa kuanzia hii leo Bocco siyo mchezaji tena wa Azam FC", Lakini
watamkumbuka kwa mengi mazuri aliyoifanyia timu hiyo mpaka ilipofikia.
Maganga maarufu kama mbunifu amesema
Bocco yuko huru kujiunga na timu yoyote hii ni baada ya kumalizika
kwa mkataba na hata mazungumzo baina yao kutofanikiwa hivyo wao
wanamtakia kila la kheri huko aendako.
Tayari kumekuwa na taarifa za mchezaji
huyo mrefu kusajiliwa na Simba taarifa ambazo bado yeye na hata viongozi
wa Simba hawajawa tayari kuzungumzia.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment