Kamishna Simon Sirro
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro
amefunguka kuwa wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala wameiba jumla ya
kete 32 za dawa za kulevya zilizokuwa kwenye mwili wa Raia wa Ghana
aliyefariki dunia akiwa katika nyumba ya wageni.
Kamanda
Sirro amesema wahudumu hao wanne wote wamekamatwa na kukiri kwamba
baada ya kifo cha raia huyo wa Ghana aliyefariki ndani ya 'Red Carpet'
iliyopo Sinza Dar es Salaam walipasua mwili wa raia huyo na kutoa kete
hizo kisha kuziuza, na kuongeza wametaja watu ambao wamewauzia ambao nao
wamekamatwa na wapo chini ya ulinzi wa polisi
"Yule Mghana ambaye alikutwa
amefariki dunia tarehe 14/ 03/ 2017 kwenye nyumba ya wageni ya 'Red
Carpet' na alichukuliwa na kupelekwa mochwari Mwananyamala lakini
inaonekana wale wahudumu wali[pata taarifa kuwa ule mwili una dawa za
kulevya, kimsingi walikula njama wakampasua na kutoa kete 32 za madawa
ya kulevya na baada ya kuyapata waliyauza hayo madawa" alisema Sirro
Kamanda Sirro aliendelea kusema kuwa mpaka sasa wanawashikilia watu wanne ambayo wamehusika katika jambo hilo.
"Mpaka sasa tunawashikilia
watu wanne ambao wanakiri kupasua mwili huo ambao ni wahusika wakuu na
ni wahudumu wa mochwari ya Mwananyamala lakini tumekwenda mbali zaidi
baada ya kufanya upasuaji wamemuuzia nani naye amekatwa pia na anaeleza
kuwa alinunua hayo madawa, lakini pia naye alichukua na kumuuzia mtu
mwingine anayefahamika kwa jina la Ally Nyundo, huyu Nyundo
tulishamkataga na kumpeleka kwa Mkemia Mkuu yeye alionekana ni mtumiaji,
kimsingi tuna hao watuhumiwa wanne na huyo wa tano aliyekamatwa sasa
tunaandaa jalada" alisisitiza Sirro
0 MAONI YAKO:
Post a Comment