
Muandishi wa habari aliyekuwa akiandika na kuripoti habari za uchunguzi
zinazohusu madawa ya kulevya na ulanguzi nchini Mexico ameuwawa.
Javier Valdez, aliyewahi kushinda tuzo mbali mbali za uandishi wa
habari zake aliuwawa siku ya jana (Jumatatau) katika mji wa Culiaciana
kaskazini mwa mji wa Sinaloa.
Watu waliokuwa na silaha walimshambulia muandishi huyo kwa kumpiga
risasa alipokuwa ndani ya gari lake wakati akiwa anaeleka kazini.
Mwandishi huyo aliyejikita katika kuandika habari hizo alikuwa akiandika
huku akijua kuwa anataraisha maisha yake.
Kwa kipindi cha miezi miwili mpaka sasa waandishi wa habari wanne
katika nchi hiyo wameuwawa. Kwa mujibu wa CPJ( Committee to Protect
Journalists)waandishi wa habari 40 waliuwawa kutokana na kurepost habari
za madawa nchini Mexico tangu mwaka 1992
0 MAONI YAKO:
Post a Comment