May 04, 2017


Unyamavu wa staa na rapper mkongwe hapa nchini Kenya kwenye muziki maarufu kama Prezzo, haujawa pingamizi kwake kutoziteka headline za vyombo vya habari.
Wiki iliyopita Prezzo amekuwa akirusha cheche kali za vitisho kwa maaadui wake haswa wale ambao wameonekana wakimnyemelea x-wake kwajina Michele Yola. Prezzo amedai kuwa Michele bado ni wake mpaka atakapo muona ameolewa. Kwahivyo hakuna rukhusa ya mtu yeyote kupiga picha au video naye bila idhini yake.
Wakati vurugu zake kwenye mitandao ikiendelea, Prezzo ameonekana mwenye jazba , na hatimaye imebainika ni nani ambaye alikuwa anamlenga. Japo hakuna ushaihidi wowote kama mtu ambaye ametishiwa maisha amewahi kuonekana kumkejeli ama kumchokoza Prezzo, Prezzo ameamua kufichua kinacho muumiza moyoni mwake. Kupitia ukurasa wake instagram, alipost picha ya mwanadada ambaye anaonekana ameinama tayari akiwa mkononi ameshika bunduki ili kulenga shabaha.
Kaka Sungura
Na chini yake kuandika caption iliyolenga moja kwa moja kwa Rapper na muasisi wa kampuni ya muziki nchini Kenya Kaka Sungura Empire maarufu kama King Kaka. Haya ndio maneno aliyoyaandika Prezzo kwenye instagram. ”prezzo254Kaka sunguch best watch his mouth my cousin sista finna take care of u #Rapcellency #TulyUnruly”
Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Facebook: Changez Ndzai
Twitter : ChangezN
Instagram:changez_ndzai

Related Posts:

  • Watu 35 wafa kwa mafuriko   Zaidi ya watu 35 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 55 wamejeruhiwa baada ya nyumba zao kuwaangukia na kuwafunika usiku wa kuamkia leo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama, mkoani Shinyanga  … Read More
  • Bajeti ya jeshi yaboreshwa China    China inasema kuwa bajeti yake ya ulinzi itaongezeka kwa asilimia kumi mwaka huu. Wanajeshi wake wanatarajiwa kupewa dola bilioni 145 na kuendelea na mfumo wa kuongeza bajeti ya jeshi ulioanza miaka 20 iliyo… Read More
  • Mwizi wa wasanii Clouds huyu hapa   Huyu kijana kushoto amekamatwa kwa kosa la kutapeli watu mbalimbali kwa kutumia majina ya wafanyakazi wa Clouds akiwemo Ruge Mutahaba na kujifanya yeye ndio kiongozi wa idara ya muziki ya Clouds fm na kuwatapeli… Read More
  • Tanzania kukumbwa na ukame   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk.Agnes Kijazi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam.  Mamlaka ya Hali ya H… Read More
  • Wanne wahukumiwa kifo MwanzaMahakama kuu ya Tanzania Mwanza imewahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa washtakiwa wanne akiwemo mume wa marehemu baada ya kupatikana na hatia ya kumuua zawadi Mangidu [22] wa kijiji cha Nyamalulu kata ya Kaseme wilayani Ge… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE