May 28, 2017

Shambulizi la kibaguzi nchini Marekani
Wanamume wawili wachomwa visu na kujeruhiwa vibaya katilka shambulizi lililoenekena kuwa na kibaguzi dhidi ya waislam katika jimbo la Portland nchini Marekani.
Mtu mmoja alisikika akiawatolea matamshi machafu wanawake wawili walioenekana kuwa waislamu na wasamaria wema kuingilia kati.
Katika tukio hilo  watu wawili walioajiru kuingilia katia tukio hilo walichomwa  visu  Ijumaa katika treni mjini Portland.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari  Portland, mtu huyo mwenye imani za kibaguzi aliacha kuwashambulia kwa maneno machafu wanawake hao na kuwashambulia watu wawili kwa visu waliokuwa wakijaribu kuwatetea wanawake hao.
Msamaria mwemo mmoja alifariki papo hapo kabla ya kufikishwa hospitali.
Alieendesha mauaji hayo alitambulika kwa jina la Jeremy Joseph Christian mwenye umri wa miaka 35.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE