June 09, 2017

31 wafariki katika shambulizi Iraq 

Takriban 31 wapoteza maisha katika mashambulizi mawili tofauti ya kujitoa mhanga nchini IraqMashambulizi mawili tofauti ya kujitoa mhanga yatekelezwa maeneo mawili tofauti nchini Iraq na kupelekea vifo vya watu 31 na 35 kujeruhiwa .

Shambulizi moja limetekelezwa katika eneo takatifu la dhehebu la Shia maeneo ya Karbala huku lingine katika soko katika mji wa Musayyib.
Daesh walitangaza kutekeleza mashambulizi yote mawili huku wakifahamisha kwamba mashambulizi hayo mawili yalitekelezwa na wanaume .
Hata hivyo afisa mmoja wa usalama alifahamisha kwamba mshambuliaji wa Musayyib alikuwa mwanamke .
Mashambulizi hayo yametekelezwa kipindi ambacho Daesh wanaendelea kushindwa Mosul.


0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE