June 09, 2017

Waziri wa mambo ya nje wa Bahrein kufanya ziara Uturuki 
Waziri wa mambo ya nje wa Bahrein sheikh Khalid ben Ahmed al-Khalifah kufanya ziara nchini Uturuki
Waziri wa mambo ya nje wa Bahrein sheikh Khalid ben Ahmed al-Khalifah anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini Uturuki hapo Jumamosi  Juni 10.
Katika zaira yake hiyo waziri huyo wa mambo ya nje wa Bahrein atakutana na rais wa Uturuki Recep Tayyıp Erdoğan.
Taarifa hiyo iliotolewa Ijumaa na wanadiplomasia baada ya kuafikiana.
Viongozi hao watazungumzia kuhusu hali inayojiri katika ukanda mzima wa Mashariki ya Kati.
Bahrein ni moja miongoni mwa mataifa ya Ghuba yaliositisha ushirikiano wake wa kidiplomasia na Qatar kwa kuituhumu kushirikiana na makundi yanayoendesha  ugaidi.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE