Akizungumza mapema asubuhi ya leo na Kituo cha Luninga cha Channel Ten
na Magic fm Radio Nabii anayekuja kwa Kasi nchini Nabii Frank leo
amefunguka na kueleza mambo makuu mawili ambayo ndiyo chanzo cha mauaji
yanayoendelea Kibiti na Rufiji na amezitaka Mamlaka husika kuyafanyia
Kazi ili kumaliza mauaji.
Amesema kwamba mauaji hayo yanatokana na sababu za Harakati za Kidini (
yaani kuna dini moja inataka kuwa ndiyo inayoaminika na kukubalika
katika huo Ukanda hivyo wanaua Watu hasa wa dini fulani ili kuwatisha na
wakimbie au wahame hayo maeneo na wabaki wao tu ) na sababu ya pili
kasema kwamba Mfumo wa Kiuchumi wa Watu wa hayo maeneo umeharibiwa hivyo
Wauwaji wameamua sasa kuwauwa wale wote ambao wanahisi ndiyo chanzo cha
Mfumo wao huu kuharibiwa. Na inasemekana kwamba Mfumo mkubwa wa
Kiuchumi au uingizaji Kipato kwa asiimia kubwa ya Watu wa hayo maeneo ni
Mkaa na kama tunavyojua Serikali imepiga marufuku huku ikiweka Sheria
kali dhidi ya wale watakaokamatwa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment