June 08, 2017

Maandamano gerezani yapelekea  7 kufarikİ Mexico 
Takriban watu 7 wafariki na wengine 13 kujeruhiwa kufuatia maandamano katika gereza moja maeneo ya Ciudad Victoria karibu na mpaka wa Marekani.
Miongoni mwa waliofariki ni polisi 4 huku polisi wengine 6 wakiwa kati ya watu walkiojeruhiwa katika maandamano hayo.
Watu walioshuhudia tukio hilo wameripoti kusikia milio ya risasi usiku wa Jumanne kuamkia siku ya Jumatano.
Mamlaka ya jela hiyo mefahamisha kwamba waligundua kwamba kulikuwa na hali ya mvutano baina ya wafungwa na kwamba baadhi ya waliokamatwa walikuwa wakiingiza silaha jela .
Luis Alberto Rodríguez ,msemaji wa mamlaka hiyo katika jimbo la Tamaulipas alifahamisha kupitia mahojiano na televisheni ya eneo hilo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE