Waziri January Makamba
Akizungumza
ofisini kwake mjini Dodoma Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,
Muungano na Mazingira, January Makamba amesema kwamba mikoa mbalimbali
nchini imekwishaanza kuathirika na hali ya jangwa na ukame ambapo vyanzo
vya maji tayari vimeshaanza kukauka, mifugo kufa ikiwa ni pamoja na
upungufu wa mvua kutokana na ukataji wa miti kiholela na migogoro baina
ya wafugaji na wakulima kutokana na kupungua kwa maeneo ya kilimo na
malisho ya mifugo.
Waziri amesema kuwa ili kukabiliana na
tatizo la ukame na jangwa nchini tayari serikali imekwishaweka mkakati
wa kupanda miti milioni 280 kila mwaka kwenye maeneo ambayo yameathirika
zaidi na jana hili la ukame.
Hata hivyo mikoa ambayo imekwisha
athirika zaidi, Waziri ameitaja ni pamoja na na Singida, Dodoma,
Shinyanga, Manyara, Simiyu, Geita na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa
Arusha.
Ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya
Kupambana na Kuenea kwa Hali ya Jangwa na Ukame Duniani ambayo
inaadhimishwa ulimwenguni kote kila ifikapo tarehe 17 Juni, kauli mbiu
ya mwaka huu ni “Ardhi ni Makazi yetu Tuitunze kwa Manufaa ya baadaye”
(‘Our Land, Our Home, Our Future’)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment