June 17, 2017

Moto mkubwa unawaka karibu na barabara mjini Pedrogao Grande 

Maafisa nchini Ureno wamesema kuwa, moto mkubwa wa msituni katika maeneo ya katikati mwa nchi hiyo, umesababisha vifo vya zaidi ya watu 25 na kuwajeruhi wengine 20, wakiwemo maafisa kadhaa wa zima moto.
Awali watu waliofariki walikuwa 19, lakini sasa idadi hiyo imepanda na kufikia 25. Wengi wao walifariki pale walipokuwa wakiukimbia mji wa Pedrogao Grande, kilomita 50 kama (Maili 30) Kusini mashariki mwa Coimbra, kwa kutumia magari yao. Hayo ni kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa serikali ya nchi hiyo.
Watatu kati yao walifariki baada ya kuvuta hewa yenye moshi mkali.
"Kwa bahati mbaya, hii inaonekana janga baya zaidi ambayo tumewahi kushuhudia katika miaka ya hivi karibuni, katika moto wa nyika," amesema Waziri mkuu Antonio Costa.
Waziri wa maswala ya ndani wa nchi hiyo João Gomes, amewaambia waandishi habari kuwa, waathiriwa 16 wameteketea ndani ya magari yao hadi kufa, pale walipokabiliwa na moto huo mkubwa katika Wilaya ya Pedrógão Grande barabara inayounganisha miji ya Figueiro dos Vinhos na Castanheira de Pera.
Moto "ulienea kwa kasi mno" katika maeneo manne, amesema Bw. Gomes.
Uhispania imetuma ndege mbili ya kuzima moto, ili kuweza kukabiliana na janga hilo.
Haijabainika kilichosababisha moto huo wa msituni, ambao umeteketeza nyumba nyingi katika maeneo hayo.Awali, meya wa eneo hilo Valdemar Alves, aliwaambia wanahabari kuwa, kuna idadi ndogo ya wazima moto, kukabiliana na janga hilo la moto katika vijiji kadhaa ambavyo vinaungua kwa sasa.na na janga hilo la moto katika vijiji kadhaa ambavyo vinaungua kwa sasa.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE