June 24, 2017

Ramani ya Pakistan 

Yamkini watu 100 wamefariki kwa kuteketea, baada ya lori moja la mafuta kupinduka na kisha kuanguka katika ajali ya barabarani.

Zaidi ya watu 100 wanaaminika walikimbia na kufika katika eneo la ajali hiyo ili kuteka mafuta yaliyokuwa yakimwagika, ndipo moto mkubwa ukawateketeza.

Ajali hiyo imetokea katika mji wa Bahawalpur nchini Pakistan.
Vyombo vya habari nchini humo, vinaripoti kuwa watu, zaidi ya 100 wamejeruhiwa ama kufa huku baadhi yao wakikimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Wazima moto wanaendelea kukabiliana na moto huo.
Taarifa ambazo bado hazijathibitishwa, zinasema kuwa lori hilo lilkuwa likiendeshwa kwa kasi ndipo likapinduka na kuanguka.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE