June 10, 2017



 
 
HABARI iliyotufikia hivi punde inaarifu kuwa Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi (pichani)

Taarifa kutoka Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ambayo imesainiwa na Mkurugenzi wake, Gerson Msigwa inaeleza kuwa Ngalamgosi amesimamishwa kazi kuanzia leo Juni 11,2017’

Mwishoni mwa wiki inayomalizika leo Mamlaka hiyo ilitoa tangazo katika vyombo vya habari ilitoa taarifa kwa umma kwamba Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imepokea maombi  ya kuongeza  muda  wa leseni  ya  kuzalisha  umeme  kutoka kwa  kampuni  ya  uzalishaji  umeme  ya Independent  Power  Tanzania  Limited (IPTL)  (“Mwombaji”).   

Hivyo basi,EWURA  ina uarifu umma  na wadau mbalimbali kwa ujumla kuwasilisha maoni au pingamizi ili kufanikisha uchambuzi mzuri wa maombi haya.

Taarifa za ilitolewa  chini  ya  kifungu  cha  19  cha  Sheria  ya  Mamlaka  ya  Udhibiti  wa  Huduma  za  Nishati  na  Maji, Sura  ya  414  ya  Sheria  za  Tanzania  na  kifungu  cha 8 cha  Sheria  ya  Umeme,  Sura  ya  131  ya  Sheria  za Tanzania.

Tayari wadadisi wa mambo wanahusisha kusimamishwa kazi huko kunatokana na tangazo hilo la kutafuta maoni ya wanachi ya kutaka kumuongezea mkataba IPTL.


Itakumbukwa kuwa Januari Mosi mwaka huu Rais Dk. John Magufuli, alitengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Felchesmi Mramba, katika hali inayoonesha kuwa Rais amekerwa na jaribio la Tanesco kupandisha bei ya umeme kuanzi.

Baada ya Mramba kutenguliwa nafasi yake alipewa Dk. Tito Esau Mwinuka kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO akimtoa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikokuwa akifundisha.


Rais Magufuli, alichukua hatua hiyo siku mbili baada ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuiidhinisha ongezeko la asilimia 8.5 ya ya bei ya huduma za umeme kwa kilichoelezwa kuwa lengo ni kukidhi gharama za uzalishaji wa umeme.

Ongezeko hilo lilitangazwa juzi jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, aliyesimamishwa kazi, Felix Ngamlagos.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE