Ikiwa ni siku moja imepita toka Rais John Pombe Magufuli apokee ripoti
ya pili ya uchunguzi wa mchanga alimaarufu kama 'Makinikia' Mbunge wa
Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kusema historia inaandikwa.
Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lissu akiteta jambo na Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe bungeni kipindi cha nyuma.
Zitto
Kabwe ameweka picha akiwa bungeni kipindi cha nyuma yeye pamoja na
Mbunge Tundu Lissu na kusema siku zote Uzalendo ni kufanya jambo ambalo
watu wengi hawakuelewi lakini wewe unajua kuwa ni jambo sahihi na
unakubali kutukanwa, kusimangwa, kuzushiwa lakini wewe unaendelea
kupambana.
Mbunge huyo anasema hata kama watu watafanya yote hayo na wewe
kuendelea kupambana ipo siku watu hao waliokuita msaliti watakuita
shujaa huku wale waliokuzomea watakushangilia
"Mwisho wa siku historia
inaandikwa tu. Uzalendo ni kufanya jambo ambalo wengi hawakuelewi lakini
wewe unajua ni jambo sahihi na unakubali kutukanwa, kususubikwa,
kusimangwa, kuzushiwa, lakini Unapambana tu. Mwisho wa siku waliokuita
msaliti watakuita shujaa. Waliokuzomea wanashangilia. Wewe unafanya
nini? Unakaa kimya kwani kwenye kukaa kimya pia kuna kusema kukubwa
zaidi. Muhimu Nchi ifaidike. Huko nyuma nilipata kusema, hata Mungu
akinichukua sasa unakwenda ukiwa umetabasamu kwani unakuwa umetimiza
wajibu wako duniani" aliandika Zitto Kabwe
0 MAONI YAKO:
Post a Comment