Wiki moja baada ya baadhi ya nchi za Gu-huba kutangaza kusitisha ushirikiano na Qatar Morocco yatuma ndege za chakula
Saudi Arabia Falme za kiarabu, Bahrein, Misri zilitangaza kusitisha ushirikiano wa kidiplomasia na Qatar.
Kufuatia
mzozo huo huo Morocco imechukua uomuzi wa kujiunga na Qatar na kutuma
ndege za chakula nchini Qatar ili kukidhi mahitaji ya raia.
Qatar imewekewa vikwazo na mataifa jirani iikituhumiwa kuunga mkono ugaidi.
Tangazo
lililotolewa na ofisi ya waziri wa mambo ya nje wa Morocco lilisema
kuwa hatua ya Morocco ya kutuma ndege hizo za chakula imechukuliwa na
mfalme Mohammed VI.
Tangazo hilo lilikumbushia kuwa mshikamano unatolewa wito hasa katika mwezi wa Ramadhan katika umma wa kiislamu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment