Serikali ya Israel imewaalika mahujaji wa Tanzania kutembelea miji yake mitakatifu kwa ada ya kiwango cha chini.
Kulingana
na mkurugenzi wa bodi ya Utalii nchini Tanzania, Devota Madachi ambaye
pamoja na katibu wa kudumu katika wizara ya mali asili na Utalii Dkt.
Aloyce Nzuki walizuru Israel kwa ziara ya siku tatu, wenyeji wao wa
Israel waliwahakikishia kuwa mahujaji wa Tanzania wataitembelea nchi
hiyo kwa ada ya chini ya kati ya dola 1,700 na dola 1,800.''Wenyeji wetu wametuambia kwamba wanataka Watanzania kutembelea taifa hilo kwa gharama ya chini''.
''Nawaomba Watanzania kutumia fursa hiyo kwa sababu mbali na uhujaji, Watanzania watakutana na wenzao wa Israel ambao watataka kuzuru maeneo ya Katavi, Mahale , Ngorongoro na Zanzibar''.
Kulingana na gazeti hilo wawekezaji wa Israel wameapa kuwekeza katika hoteli za kifahari nchini Tanzania.
''Kwa ufupi hii imekuwa ziara ya kufana kwa pande zote mbili'', alisema.
Gazeti hilo lilimnukuu balozi wa Tanzania nchini Israel bwana Job Massima, akisema kuwa mkutano huo ni wake wa kwanza tangu kuwasilisha ripoti kwamba ulimsaidia kujua ni kwa nini Waisrael wanawapenda Watanzania.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment