Kukamilika kwa
mwezi mtukufu wa Ramadan ni likizo kuu ya kidini ya Eid al-Fitr, ambapo
waislamu kote duniani hukusanyika kwa sherehe za kumaliza mwezi
mtukufu.
Hata hivyo wakati wa siku kuu hiyo kubwa takatifu ya
kiislamu inapowadia, wengi wa waislamu bilioni 1.8 huwa na matumaini
kupata ishara ya kushiriki sherehe hizo.Waislamu hufuata kalenda inayoambatana na mwezi.
Ikiwa mwezi huu ungefuata kalenda ya jua, watu ambao wanaishi sehemu fulani za dunia wangesherehekea Ramadan yao msimu ya joto huku wakiwa na siku ndefu ya jua, huku sehemu zingine za dunia zikiwa na vipindi vifupi vya misimu ya baridi.
Waislamu kwenye nchi nyingi hutegemea habari kuhusu kuonekana kwa mwezi mpya badala ya kuangalia angani wao wenyewe
Watoto baad ya swala ya EIDD nchini Kenya june 25
Kwa hivyo tarehe za Eid hutofautiana kote duniani, licha ya kuwepo tofauti ya siku moja au mbili hivi.
Kwa mfano mamlaka nchini Saudi Arabia, yenye waislamu wengi wa Sunni, hutangaza kumalizika mwezi wa Ramadan, kutokana na maoni ya watu ambao huona mwezi mpya.
Lakini nchini Iran yenye waislamu wengi wa Shia hutegemea matangazo ya serikali.
Makala hii imeandaliwa na Shirika la Habari la Uingereza BBC
0 MAONI YAKO:
Post a Comment