June 24, 2017



بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ


Tunapenda kuwaarifu kuonekana kwa mwezi mpya wa Shawwaal leo hii Jumamosi 29 Ramadhwaan 1438H katika nchi mbalimbali duniani, Baadhi ya nchi ambazo umeonekana ni pamoja na Saudiarabia, Yemen,Oman,Australia, Indonesia nk Kwa hiyo, kesho Jumapili (25 June 2017M) In shaa Allaah ni tarehe 1 Shawwaal 1438H, na ndio Sikukuu yetu ya ‘Iydul-Fitwr.

Kwa munaasabah huu wa ‘Iyd Al-Fitwr tunapenda kuchukua fursa hii kuwasilisha salaam zetu za siku hii na du'aa njema kwenu wote, tukimuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Atutaqabalie 'amali zetu na zenu  ‘TAQABBALA ALLAAHU MINNAA WA MINKUM’  (Hivi ndivyo Maswahaba watukufu walivyokuwa wakiambiana pindi wanapokutana katika siku ya 'Iyd). Na tunamuomba Yeye Aliyetukuka na Mweza, Awajaalie furaha, amani, mapenzi, siha, iymaan, taqwa, ikhlaasw pamoja na karama na utukufu katika masiku yote ya uhai wetu.


Hali kadhaalika tunapenda kuwakumbusha na kuwapa nasaha ya kuifufua Sunnah iliyosahauliwa ya kuleta Takbiyrah  inayotakiwa kusomwa kuanzia usiku wa ‘Iyd  (baada ya kumaliza kufunga Swawm ya siku ya mwisho ya Ramadhwaan)  mpaka asubuhi anapoingia Imaam kuswalisha Swalaah ya ‘Iyd.

Na inapasa kuwakumbusha ndugu wengine ili kila mmoja apate thawabu za kuifufua Sunnah hii ambayo wengi wameiacha. Tuanze kukumbusha familia zetu majumbani mwetu kuitekeleza Sunnah hii tukufu. Thawabu hizo zitazidi kuongozeka kwa yule atakayeanza kumfunza mwenziwe na ataendelea kuchuma thawabu tele kila mafunzo hayo yatakapoendelea kufunzwa: Anasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): 

مَنْ سَنَّ فِي الْإِسْلَامِ سُنَّةً حَسَنَةً فَعُمِلَ بِهَا بَعْدَهُ كُتِبَ لَهُ مِثْلُ أَجْرِ مَنْ عَمِلَ بِهَا ، وَلَا يَنْقُصُ مِنْ أُجُورِهِمْ شَيْءٌ.... أخرجه مسلم في صحيحه
((Atakayefanya kitendo kizuri katika Uislam atapata ujira wake na ujira wa yule atakayekitenda baada yake  bila ya kupungukiwa thawabu zao chochote…)) [Muslim]




Chanzo:alhidaaya.com

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE