Serikali ya China imetangaza habari ya kufukiwa
watu 140 katika maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kali
katika maeneo ya kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Taarifa
iliyotangazwa leo na China imesema kuwa, maporomoko ya ardhi yametokea
katika mkoa wa Sichuan ambapo jumla ya nyumba 40 ambazo walikuwa
wanaishi ndani yake watu 140 zimefukiwa na udongo. Kwa mujibu wa habari
hiyo, wafanyakazi wa kutoa misaada wametumwa kwenda eneo hilo na kuanza
kutafuta miili ya wahanga wa ajali hiyo.Siku chache zilizopita, mamlaka ya hali ya hewa kwa kushirikiana na
idara ya kukabiliana na mafuriko na majanga ya kimaumbile nchini China
sambamba na kuonya juu ya hali hiyo, zilitangaza kuwepo uwezekano wa
kunyesha mvua kali katika maeneo tofauti ya nchi hiyo yakiwamo ya kusini
magharibi. Aidha mvua ambazo zimekuwa zikinyesha katika miezi ya Mei,
Juni na Julai zimekuwa zikisababisha hasara kubwa za mali na roho
hususan katika maeneo ya kusini mwa nchi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment