Nyumba aliyokuwa akiishi malkia wa muziki wa pop duniani Madonna
katika kipindi cha utoto wake akiwa pamoja na wazazi wake imeingizwa
sokoni.
Nyumba hiyo ambayo ipo katika mji wa Detroit katika jimbo la Michigan
nchini Marekani, iliungua kwa moto mwaka 2008 na iliachwa wazi mpaka
kufikia mwaka 2012 ndipo ilipouzwa kwa kiasi cha shilingi milioni
205,041,035 kwa fedha za kitanzania.
Lakini kwa sasa nyumba hiyo yenye vyumba vitano vya kulala, mabafu
matatu, ambayo ilitengenezwa vizuri na mwenye nyumba huyo mpya inauzwa
kwa kiasi cha dola 479,900 ambapo kwa fedha za kibongo ni sawa na
shilingi 1,073,226,252.
Hizi ni baadhi ya picha za nyumba hiyo.
Na Laila Sued
0 MAONI YAKO:
Post a Comment